Amnesty International yamkosoa kansela mtarajiwa wa Ujerumani kwa kumwalika Netanyahu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i123254-amnesty_international_yamkosoa_kansela_mtarajiwa_wa_ujerumani_kwa_kumwalika_netanyahu
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limemkosoa vikali Friedrich Merz kansela mtarajiwa wa Ujerumani kwa kumualika Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni kuitembelea Ujerumani.
(last modified 2025-02-26T23:46:46+00:00 )
Feb 26, 2025 23:46 UTC
  • Amnesty International yamkosoa kansela mtarajiwa wa Ujerumani kwa kumwalika Netanyahu

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limemkosoa vikali Friedrich Merz kansela mtarajiwa wa Ujerumani kwa kumualika Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni kuitembelea Ujerumani.

Amnesty International imeitaja hatua hiyo ya mgombea wa ukkansela wa Ujerumani na ambaye anapewa nafasi kubwa ya kushinda kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.

Sambamba na kumkosoa kiongozi huyo wa chama cha Christian Democratic Union, shirika hilo la haki za binadamu limesema katika taarifa yake kwamba:

Si mwanzo mzuri kama kansela mtarajiwa: Katika mkesha wa uchaguzi wa Bunge (Bundestag), Friedrich Merz anaonekana kumwalika Benjamin Netanyahu nchini Ujerumani, ambaye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imetoa hati ya kukamatwa kwake.

Sehemu nyingine ya taarifa ya Amnesty International imesema, hatua hii ni sawa na "wito wa wazi" wa kukiuka sheria na kusisitiza kwamba serikali mpya ya Ujerumani lazima iheshimu sheria za kimataifa na taasisi za haki za binadamu bila unafiki na undumakuwili.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel anatuhuumiwa kutenda jinai za kivita na dhidi ya binadamu katika Ukanda wa Gaza

 

Mwezi Novemba mwaka jana (2024), Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilitoa hati za kukamatwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na na aliyekuwa waziri wake wa vita Yoav Gallant baada ya kuwafungulia mashtaka ya kutenda jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu huko Gaza, ambako utawala wa Kizayuni uliendesha vita vya kinyama na kufanya mauaji ya kimbarii tangu mwezi wa Oktoba mwaka 2023.