Putin apendekeza mazungumzo ya moja kwa moja na Ukraine kwa ajili ya 'amani ya kudumu'
(last modified Mon, 12 May 2025 02:01:06 GMT )
May 12, 2025 02:01 UTC
  • Putin apendekeza mazungumzo ya moja kwa moja na Ukraine kwa ajili ya 'amani ya kudumu'

Rais Vladimir Putin wa Russia ametoa wito akitaka kuanza tena mazungumzo ya moja kwa moja bila masharti kati ya nchi yake na Ukraine mjini Istanbul, Mei 15, ili kufikia makubaliano ya amani ya kudumu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu kuhusu rais Putin ameashiria mazungumzo ya amani yaliyofeli yaliyofanyika mwezi Machi 2022 mjini Istanbul, Uturuki muda mfupi baada ya Moscow kuanzisha oparesheni maalumu ya kijeshi dhidi ya Ukraine na kupendekeza kuanza tena mazungumzo hayo. 

Rais wa Russia ameongeza kuwa tumedhamiria kufanya mazungumzo ya jadi na Ukraine na tunawapendekezea viongozi wa Kiev kuanza tena mazungumzo siku ya Alhamisi. 

Rais Vladimir Putin amesema kuwa uamuzi sasa upo upande wa mamlaka husika za Ukraine ambao inaonekana, wanaongozwa na matashi ya kibinafsi ya kisiasa, na sio maslahi ya watu wao.

Dmitry Peskov, Msemaji wa Ikulu ya Rais wa Russia (Kremlin) amesema kuwa 'hili ni pendekezo muhimu sana, ambalo linathibitisha nia ya kweli ya Moscow kupatikana suluhisho la amani.”