Kimbunga, maporomoko ya ardhi yaua 40 Mexico
https://parstoday.ir/sw/news/world-i12838-kimbunga_maporomoko_ya_ardhi_yaua_40_mexico
Makumi ya watu wameuawa kufuatia kimbunga kikali, maporomoko ya ardhi na mvua zinazoendelea kunyesha mashariki mwa Mexico.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 08, 2016 03:06 UTC
  • Kimbunga, maporomoko ya ardhi yaua 40 Mexico

Makumi ya watu wameuawa kufuatia kimbunga kikali, maporomoko ya ardhi na mvua zinazoendelea kunyesha mashariki mwa Mexico.

Taarifa ya serikali ya nchi hiyo imesema kuwa, watu zaidi ya 30 wamepoteza maisha katika majanga hayo ya kimaumbile yaliyosababishwa na kimbunga cha Earl katika mji wa Huauchinango, katikati mwa jimbo la Puebla.

Taathira hasi za Kimbunga cha Earl nchini Mexico

Habari zaidi zinasema kuwa, watu wengine 10 wameaga dunia kutokana na maporomoko ya ardhi katika Ghuba ya Veracruz, pwani ya nchi hiyo ya Amerika ya Latini.

Gabriel Alvarado, Meya wa mji wa Huauchinango amesema mamia ya watu wameathiriwa na majanga hayo katika mji huo sambamba na kuharibiwa miundomsingi na nyenzo za mawasiliano.

Ramani inayoonyesha kusambaa kwa Kimbuga cha Earl Amerika ya Latini

Alkhamisi iliyopita, Kimbunga Cha Earl kilisababisha vifo vya watu 9 katika nchi za Haiti na Jamhuri ya Dominican huko Amerika ya Latini.