Microsoft inachunguza teknolojia yake kutumiwa na Israel kuwafanyia ujasusi Wapalestina
-
Jeshi la Israel linatumia data za kampuni ya Microsoft kuwafanyia ujasusi Wapalestina
Kampuni ya Microsof imeanza kufanya uchunguzi kuhusiana na taarifa kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia teknolojia ya kampuni hiyo kwa ajili ya kuwafanyia ujasusi Wapalestina.
Gazeti la The Guardian la Uingereza limeripoti kuwa, kampuni ya Microsoft imeanzisha uchunguzi wa dharura kuhusiana na madai kwamba, utawala ghasibu wa Israel umetumia teknolojia ya kampuni hiyo kuwafuatilia Wapalestina.
Uchunguzi huu unachunguza matumizi ya jukwaa la Microsoft na kitengo cha kijasusi cha jeshi la Israel cha 8200 kuhifadhi mazungumzo ya Wapalestina.
Microsoft pia imeelezea wasiwasi wake juu ya ripoti zinazoonyesha kwamba, huduma za kijasusi za Israel zimetumia mazungumzo haya yaliyorekodiwa kwenye jukwaa la kampuni kutambua na kulipua shabaha huko Gaza.
Gazeti la Uingereza la The Guardian hapo awali lilifichua, likinukuu vyanzo katika kitengo cha 8200 cha jeshi la Israel, kwamba data kutoka katika jukwaa la wingu la Microsoft la Azure lilikuwa linatumika kama hifadhidata kubwa ya wakaazi wa Ukingo wa Magharibi.
Vyanzo hivi vilisisitiza kuwa, maelezo haya yalitumiwa kwa madhumuni kama vile kuwatishia na kudai pesa ili wasitoe taarifa zao, kuwaweka kizuizini au kuhalalisha mauaji yao.
Pia imesemekana kuwa data hizi zilikuwa na nafasi muhimu katika kupanga mashambulizi ya kijeshi ya utawala wa Israel huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Akizungumzia sula hili, msemaji wa Microsoft alidai kuwa kampuni hiyo haina taarifa kuhusu aina ya data iliyohifadhiwa na kitengo cha 8200 cha jeshi la Israel