Ubelgiji: Tunaunga mkono vikwazo vyovyote vinavyopendekezwa vya EU dhidi ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i130894-ubelgiji_tunaunga_mkono_vikwazo_vyovyote_vinavyopendekezwa_vya_eu_dhidi_ya_israel
Waziri Mkuu wa Ubelgiji ametangaza kuwa, nchi yake inaunga mkono vikwazo vyovyote vitakavyopendekezwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya Israel.
(last modified 2025-09-17T06:46:14+00:00 )
Sep 17, 2025 06:46 UTC
  • Ubelgiji: Tunaunga mkono vikwazo vyovyote vinavyopendekezwa vya EU dhidi ya Israel

Waziri Mkuu wa Ubelgiji ametangaza kuwa, nchi yake inaunga mkono vikwazo vyovyote vitakavyopendekezwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya Israel.

Shirika la Habari la Mehr limetoa taarifa hiyo na kuongeza kuwa, Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Alexander De Croo amesema: "Tunaunga mkono mapendekezo yoyote ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Israel bila ya kufanya majadiliano yoyote."

Matamshi hayo ya Waziri Mkuu wa Ubelgiji yametolewa wakati Tume ya Uchunguzi ya Kimataifa yenye uhusiano na Umoja wa Mataifa ikitangaza jana Jumanne kwamba utawala wa Kizayuni umefanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza. Tume hiyo imetumia neno lenyewe hasa la mauaji ya kimbari kwenye taarifa yake hiyo ya jana.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa, viongozi wa utawala wa Kizayuni na madola yenye mafungamano nao wamefanya mauaji matano ya kimbari huko Ghaza.

Utawala wa Kizayuni umekuwa ukifanya jinai za kutisha dhidi ya watoto, wanawake na vizee wa Palestina kwa muda wa miaka 2 sasa kwa lengo la kuwaangamiza Wapalestina kwa kuwatesa kwa njaa hasa huko Ghaza. Kuna aina 60,000 za ushahidi na vidhibiti vimekusanywa kuutia hatia utawala katili wa Kizayuni wa Israel.