Ireland yataka Israel na wafadhili wake watimuliwe Umoja wa Mataifa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i130896-ireland_yataka_israel_na_wafadhili_wake_watimuliwe_umoja_wa_mataifa
Rais wa Ireland ametoa mwito wa kufukuzwa na kutimuliwa kwenye Umoja wa Mataifa, utawala wa Kizayuni na wafadhili wake wanaoisheheneza silaha Israel.
(last modified 2025-09-17T06:46:41+00:00 )
Sep 17, 2025 06:46 UTC
  • Ireland yataka Israel na wafadhili wake watimuliwe Umoja wa Mataifa

Rais wa Ireland ametoa mwito wa kufukuzwa na kutimuliwa kwenye Umoja wa Mataifa, utawala wa Kizayuni na wafadhili wake wanaoisheheneza silaha Israel.

Kwa mujibu wa televisheni ya Al Jazeera, Rais Michael D. Higgins wa Ireland amesema kuwa Israel na nchi zinazoiunga mkono zinapaswa kufukuzwa na kutolewa nje ya Umoja wa Mataifa.

Ameongeza kuwa, hatupaswi kulegeza tena msimamo katika suala zima la kukomesha kuipa silaha Israel na kukabiliana pia na wahusika wa uhalifu huu dhidi ya wanadamu wenzetu huko Palestina.

Rais wa Ireland aidha amesema: Baadhi ya nchi zenye nguvu za Umoja wa Ulaya zimeendelea kunyamazia kimya mateso na njaa ya watoto waliodhoofika na waliokonda vibaya kutokana na maafa ya kibinadamu yanayosababishwa na Israel huko Ghaza.

Kabla ya hapo, Waziri Mkuu wa Ireland, Michael Martin alisema katika hotuba yake kwamba, ni lazima tuzidishe mashinikizo ya kimataifa dhidi ya Israel ili kukomesha jinai zake kwenye Ukanda wa Ghaza. 

Kamisheni ya Kimataifa ya Uchunguzi inayofanya kazi chini ya Umoja wa Mataifa ilitangaza jana Jumanne kwamba utawala wa Kizayuni unafanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza. Tume hiyo imetumia rasmi na moja kwa moja neno mauaji ya kimbari.

Utawala wa Kizayuni umekuwa ukifanya mauaji ya umati dhidi ya Wapalestina kwa muda wa miaka 2 sasa kwa lengo la kuwaangamiza Wapalestina wote na kuwatesa kwa njaa hasa wa Ukanda wa Ghaza. Kuna aina 60,000 za ushahidi na vidhibiti zimekusanywa kutilia nguvu uhakika huo.