Guterres: Mwenendo wa vita wa Israel huko Gaza 'kimsingi si sahihi'
https://parstoday.ir/sw/news/world-i133908-guterres_mwenendo_wa_vita_wa_israel_huko_gaza_'kimsingi_si_sahihi'
Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani namna Israel ilivyoendesha vita dhidi ya Gaza na kuutaja mwenendo huo kuwa kimsingi si sahihi. Amesema, kuna sababu kubwa" za kuamini kwamba wanajeshi wa Israel wametenda jinai za kivita katika ardhi ya Palestina.
(last modified 2025-12-04T10:49:36+00:00 )
Dec 04, 2025 07:46 UTC
  • Antonio Guterres Katibu Mkuu wa UN
    Antonio Guterres Katibu Mkuu wa UN

Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani namna Israel ilivyoendesha vita dhidi ya Gaza na kuutaja mwenendo huo kuwa kimsingi si sahihi. Amesema, kuna sababu kubwa" za kuamini kwamba wanajeshi wa Israel wametenda jinai za kivita katika ardhi ya Palestina.

Guterres amebainisha haya jana Jumatano katika mahojiano na Mhariri Mkuu wa Shirika la Habari la Reuters Alessandra Galloni  huko New York.

"Nadhani kulikuwa na suala ambalo kimsingi si sahihi kuhusu vita vilivyoendeshwa huku kukiwa na upuuzaji kikamilifu kuhusiana na  vifo vya raia na uharibifu uliosababishwa huko Gaza." amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. 

Katika mahojiano hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa lengo lilikuwa kuiangamiza Hamas. Gaza imeharibiwa lakini harakati ya Hamas haijaangamizwa.  

Alipoulizwa kama anaamini kuwa wanajeshi wa Israel wanaweza kuwa na hatia ya kutenda jinai za kivita tangu mzozo huo uanze zaidi ya miaka miwili iliyopita, Guterres amesema "kuna sababu kubwa za kuamini kwamba uwezekano huo unaweza kuwa ukweli".

Danny Danon Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa amejibu matamshi haya ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akimtuhumu kuwa anatumia nafasi yake ya juu kwa kuilaumu na kuilaani Israel na Waisraili katika kila fursa.