Rais wa Belarus: Wavamizi Marekani na Israel hawajafikia malengo yao
https://parstoday.ir/sw/news/world-i137356-rais_wa_belarus_wavamizi_marekani_na_israel_hawajafikia_malengo_yao
Rais Alexender Lukashenko wa Belarus amelaani mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran na kusema kuwa wavamizi hao hawajifikia hata lengo lao moja.
(last modified 2026-03-14T03:45:55+00:00 )
Mar 14, 2026 03:45 UTC
  • Alexender Lukashenko
    Alexender Lukashenko

Rais Alexender Lukashenko wa Belarus amelaani mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran na kusema kuwa wavamizi hao hawajifikia hata lengo lao moja.

Rais Lukashenki amesema: Hivi sasa ambapo Rais Donald Trump wa Marekani anadai kuwa “tumelipua kila kitu nchini Iran na hatuna tena kazi huko”, kwa hakika hizi ni juhudi za kutaka kujinasua vitani.

Lukashenko ameongeza kuwa: "Kuhusu suala hilo Trump amesema sawa. Hilo ni chaguo bora zaidi. Acha wajigambe kwamba wamepiga kila kitu lakini waondoke vitani; kwa sababu hali ya mambo itakuwa mbaya sana kwao iwapo vita vitaendelea."

Rais wa Belarus amesema Iran ni nchi kubwa sana yenye watu waliopevuka kwenye masuala ya kimaanawi na kiroho na Waislamu na kuongeza kuwa: Mashambulizi dhidi ya Iran yamewaunganisha wananchi licha ya hitilafu mbalimbali za kisiasa.