Maandamano ya kuunga mkono Iran kutoka London hadi Auckland
https://parstoday.ir/sw/news/world-i137814-maandamano_ya_kuunga_mkono_iran_kutoka_london_hadi_auckland
Maandamano ya kulaani hujuma za kijeshi za Washington na Tel Aviv dhidi ya Iran yangali yanaendelea katika pembe mbalimbali za dunia.
(last modified 2026-04-06T02:09:01+00:00 )
Apr 06, 2026 02:09 UTC
  • Maandamano ya kuunga mkono Iran kutoka London hadi Auckland

Maandamano ya kulaani hujuma za kijeshi za Washington na Tel Aviv dhidi ya Iran yangali yanaendelea katika pembe mbalimbali za dunia.

Maandamano na mikusanyiko mikubwa ya watu imekuwa ikifanyika katika miji mbalimbali ya Ulaya ikiwemo ya Genoa nchini italia na London Uingereza kwa madhumuni ya kulaani hujuma za Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Maandamano ya wapinzani wa vita na kuwatetea watu wa Iran, Lebanon na Palestina pia yamefanyika katika mji wa Cork, Ireland. Washiriki wametoa wito wa kusimamishwa vita mara moja, mashambulizi ya mabomu na mauaji ya watu wasio na hatia yanayofanywa na utawala wa Kizayuni na Marekani katika nchi zilizotajwa. Waandamanaji wakiwa wamebeba bendera za Iran, Hizbullah ya Lebanon na Palestina wamepiga nara za kupinga vikali vita.

Huku hujuma za kijeshi za Marekani na Israel dhidi ya Iran zikiendelea, wimbi la maandamano ya kupinga vita pia limeibuka huko New Zealand. Waandamanaji walikusanyika siku ya Jumamosi katika uwanja wa Te Komititanga katikati mwa mji wa Auckland katika kulaani kimya cha serikali ya Waziri Mkuu Christopher Luxon na kutochukua kwake hatua kuhusu "vita haramu na vya kichokozi" dhidi ya Iran.

Huku wakilaani mauaji ya kimbari huko Gaza, wazungumzaji katika maandamano hayo wamekosoa vikali kutokuwepo msimamo wa msingi wa serikali ya New Zealand kuhusu vita vya hivi sasa dhidi ya Iran. Wameitaja Iran kuwa mmoja wa waungaji mkono wakuu wa "haki ya kujitawala na kutendewa haki Wapalestina." Wameitaka serikali ya New Zealand ijitenge na sera za kidhalimu na mabavu za Marekani na Israel.