Wahajiri waendelea kuokolewa majini katika bahari ya Mediterania
Mshirika ya misaada ya kibinadamu yameripoti kuwa juma la wahajiri 700 wamenusurika kifo baada ya kuopolewa katika bahari ya Mediterania.
Shirikisho la Kimataifa la Jumuiya za Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu jana Jumapili zilitoa taarifa yao zikibainisha kuwa, wahajiri 700 waliokuwa wamepakia kwenye boti zilizo dhaifu kusini mwa bahari ya Mediterania wamenusurika kifo. Watoto wadogo kadhaa wanaonyonya ni miongoni mwa wahajiri hao walionusurika kifo, ambapo baadhi yao wametajwa kuwa na umri wa karibu miezi mitatu au minne.
Takwimu mpya za Shirika la Wahajiri Duniani zinaonyeshah kuwa tangu kuanza mwaka huu wa 2016 hadi sasa, wahajiri karibu laki moja na elfu tano; ambao wengi walitokea Libya walifanikiwa kuingia nchini Italia. Katika kipndi hicho wanaume, wanawake na watoto 2726 pia walizama majini kabla ya kufika katika nchi waliyokuwa wakielekea.