Oct 01, 2024 06:24 UTC
  • Israel yashambulia kwa mabomu makazi ya wakimbizi wa Kipalestina Gaza

Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zimeshambulia kwa mabomu shule ya makazi ya Wapalestina katika mji wa Gaza.

Shirika la habari la IRNA limesema katika ripoti yake  kuwa, mashambulizi ya  ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zimefanya mauaji ya kinyama dhidi ya raia 6 wa Kipalestina katika mashambulio hayo yya mabomu katika shule inayowahifadhi wakimbizi wa Kipalestina katika kitongoji cha "Al-Tufah" mashariki mwa Ukanda wa Gaza.

Shambulio la usiku kwenye makazi ya wakimbizi huko Ukanda wa Gaza Wapalestina 6 wauawa shahidi 

Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, utawala bandia wa Kizayuni umeshafanya mauaji makubwa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya watu wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina kwa uungaji mkono kamili wa nchi za Magharibi mshirika wake mkuu ikiwa ni Marekani. 

Wajuzi wa mambo wanaaamini kuuwa, kimya cha jumuiya ya kimataifa na taasisi za kutetea haki za binadamu kuhusiana na jinai za utawala ghasibu wa Israel kimesababisha kuendelea kwa mauaji ya wanawake na watoto wa Kipalestina yanayofanywa na jeshi la utawala haramu wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa tangazo la Wizara ya Afya ya Palestina, idadi ya mashahidi huko Ukanda wa  Gaza tangu kuanza kwa mashambulio ya kinyama yay Israel imefikia watu elfu 41, 615 na idadi ya watu waliojeruhiwa imefikia watu 96, 359.

Tags