Kuongezeka pakubwa mashambulizi dhidi ya Misikiti na Waislamu nchini Ujerumani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i18013-kuongezeka_pakubwa_mashambulizi_dhidi_ya_misikiti_na_waislamu_nchini_ujerumani
Ripoti mpya iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha kuongezeka kwa kiasi kikubwa mashambulizi dhidi ya Waislamu na misikiti huko Ujerumani.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Oct 23, 2016 11:38 UTC
  • Kuongezeka pakubwa mashambulizi dhidi ya Misikiti na Waislamu nchini Ujerumani

Ripoti mpya iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha kuongezeka kwa kiasi kikubwa mashambulizi dhidi ya Waislamu na misikiti huko Ujerumani.

Gazeti la Ujerumani la Tag Spiegel limeandika kuwa polisi ya nchi hiyo imesajili visa 28 vya kushambuliwa misikiti nchini humo tangu mwanzoni mwa mwezi Juni  mwaka huu kote nchini humo. Ripoti hiyo imeongeza kuwa mwaka 2014, visa karibu 24 vya kushambuliwa misikiti huko Ujerumani viliripotiwa na mwaka jana wa 2015 kulikuwa na visa 75 na mwaka huu kumeripotiwa mashambulizi 52 dhidi ya misikiti huko Ujerumani.

Msikiti ulioshambuliwa kwa kuchomwa moto huko Ujerumani

Monica Lazar mbunge wa chama cha Kijani katika bunge la Ujerumani amezungumzia matukio hayo ya kushambuliwa misikitiki na Waislamu nchini humo na kueleza kuwa, huo ni uthibitisho wa kuogofya wa chuki zinazoongezeka dhidi ya Uislamu huko Ujerumani. Mashambulizi halisi yanayotekelezwa dhidi ya Waislamu na taasisi zenye mfungamano nao huko Ujerumani ni wazi kuwa ni zaidi ya haya yanayoripotiwa. Hii ni kwa sababu, mameya wa miji nchini humo hawatoi taarifa kwa polisi kuhusu hujuma na uhalifu wote wa aina hiyo. 

Waislamu wakiandamana kupinga chuki dhidi ya Uislamu nchini Ujerumani