EU yaonya kuhusu hatari ya vita vya Russia, Uturuki
https://parstoday.ir/sw/news/world-i1837-eu_yaonya_kuhusu_hatari_ya_vita_vya_russia_uturuki
Mkuu wa Sera za Kigeni katika Umoja wa Ulaya ameonya kuhusu uwezekano wa kuzuka vita baina ya Russia na Uturuki.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 24, 2016 04:12 UTC
  • EU yaonya kuhusu hatari ya vita vya Russia, Uturuki

Mkuu wa Sera za Kigeni katika Umoja wa Ulaya ameonya kuhusu uwezekano wa kuzuka vita baina ya Russia na Uturuki.

Federica Mogherini Mkuu wa Sera za Kigeni katika Umoja wa Ulaya ameyasema hayo alipohutubu katika Kamati ya Kigeni ya Bunge la Ulaya. Aliongeza kuwa, Ulaya inatazama vita vya Syria kama vita vya niaba baina ya madola yenye ushawishi katika eneo. Ameongeza kuwa, kuna uwezekano wa vita hivi kubadilika na kuwa kadhia kubwa zaidi.

Mogherini amesema vita vijavyo havitakuwa baina ya Russia na Marekani bali vinaweza kuwa baina ya Uturuki na Russia.

Mkuu wa Sera za Kigeni Umoja wa Ulaya amongeza kuwa, Ulaya inataka kuchukua hatua za kupunguza malumbano eneo la Mashariki ya Kati.

Katika miezi ya hivi karibuni kumeshuhudiwa msuguano mkubwa baina ya Russia na Uturuki kuhusu vita vya Syria. Russia imetuma ndege zake za kivita kukabiliana na magaidi wa ISIS au Daesh Syria huku serikali ya Damascus ikiituhumu Uturuki kuwa inawaunga mkono magaidi wanaotaka kuiangusha serikali ya Damascus.