Majimbo ya Texas na California yataka kujitenga na Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i19414-majimbo_ya_texas_na_california_yataka_kujitenga_na_marekani
Majimbo ya Texas na California yanataka kujitenga na Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 14, 2016 00:39 UTC
  • Majimbo ya Texas na California yataka kujitenga na Marekani

Majimbo ya Texas na California yanataka kujitenga na Marekani.

Toleo la jana la gazeti la USA Today limeripoti kuwa kufuatia ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa Marekani wananchi katika baadhi ya majimbo ya nchi hiyo yakiwemo ya Texas na California wamezungumzia suala la kujitangazia uhuru na kujitenga na Marekani.

Katika siku za karibuni, baadhi ya makundi yanayopigania kujitawala jimbo la California wamekuwa wakizungumzia suala la kujitenga jimbo hilo na Marekani 'CalExit'.

Kwa mujibu ya ripoti ya USA Today suala hilo limepewa kipaumbele na wananchi wa jimbo la California na wa majimbo ya magharibi mwa Marekani ambao wameudhika kutokana na kushindwa Hillary Clinton aliyegombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrats.

Hillary Clinton, aliyegombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrats

Watu wengi wa jimbo la California wameanzisha kampeni katika mtandao wa kijamii wa Twitter ijulikanayo kama 'CalExit' (Kujitoa California Kwenye Muungano wa Majimbo ya Marekani- USA).

Ripoti ya gazeti la USA Today imebainisha pia kuwa, kufuatia kutangazwa ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa Marekani, tovuti ya Wizara ya Uhajiri ya Canada haikuweza kupatikana kwa muda wa saa kadhaa kutokana na wimbi kubwa la raia wa Marekani waliokuwa wakiwasilisha maombi ya kutaka kwenda kuishi nchini humo.../