Trump: Tutawafunga jela au kuwatimua wahajiri milioni 3
https://parstoday.ir/sw/news/world-i19432-trump_tutawafunga_jela_au_kuwatimua_wahajiri_milioni_3
Hata kabla ya kuapishwa, Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameahidi kutekeleza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi, likiwemo suala la kuwatimua wahamiaji nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 14, 2016 04:31 UTC
  • Trump: Tutawafunga jela au kuwatimua wahajiri milioni 3

Hata kabla ya kuapishwa, Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameahidi kutekeleza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi, likiwemo suala la kuwatimua wahamiaji nchini humo.

Katika mahojiano na shirika la habari la CBS, Trump amesema mara tu atakapokabidhiwa uongozi wa nchi mapema mwakani, ataanzisha mara moja mchakato wa kuwafunga jela au kuwafukuza nchini humo wahamiaji haramu wapatao milioni 3 ambao hawajasajiliwa, haswa wenye rekodi za kufanya uhalifu.

Hii ni katika hali ambayo, tovuti ya habari ya Middle East imeripoti kuwa, mashambulizi ya wafuasi wa Trump kwa wanawake kadhaa wa Kiislamu nchini humo baada ya ushindi wa mgombea huyo wa kiti cha rais yamewatia woga wanawake wengine wa Kiislamu kuhudhuria katika mijumuiko ya umma.

Ukandamizaji wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi

Katika kampeni zake za uchaguzi, Trump aliweka wazi misimamo yake mikali iliyo dhidi ya wahamiaji, Wamarekani wenye asili ya Afrika na Waislamu na kutoa wito wa kutumiwa mbinu za dikteta wa zamani wa Ujerumani Adolph Hitler dhidi ya watu hao.

Kadhalika bilionea huyo wa chama cha Republican katika kile wadadisi wa mambo wanahisi ni dhihaka na kejeli, ameiambia CBS kuwa, ikiwezekana kisheria, atapokea mshahara wa dola 1 ya Marekani kwa mwaka, badala ya dola 400,000 kwa mwezi kama ilivyo sasa.