Russia: Wasyria wenyewe watainisha hatima ya nchi yao
https://parstoday.ir/sw/news/world-i1951-russia_wasyria_wenyewe_watainisha_hatima_ya_nchi_yao
Spika wa Bunge la Duma la Russia amesema kuwa hakuna nchi yenye haki ya kuainisha hatima ya Syria badala ya Wasyria wenyewe.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 25, 2016 23:36 UTC
  • Russia: Wasyria wenyewe watainisha hatima ya nchi yao

Spika wa Bunge la Duma la Russia amesema kuwa hakuna nchi yenye haki ya kuainisha hatima ya Syria badala ya Wasyria wenyewe.

Sergey Naryshkin ameuambia mkutano wa mabunge wa Shirika la Usalama na Ushirikiano wa Ulaya mjini Vienna kwamba, hakuna nchi yenye haki ya kuwachukulia maamuzi wananchi wa Syria hata kama itakuwa na nguvu na ushawishi mkubwa kupita kiasi. Naryshkin ameongeza kuwa, Russia na Marekani zimeunga mkono mpango wa kusitisha vita nchini Syria lakini mpango huo hauhusu makundi ya kigaidi.

Spika wa Duma pia amezitaka nchi wanachama katika Shirika la Usalama na Ushirikiano wa Ulaya kuheshimu misingi ya shirika hilo. Amesema msingi wa jumuiya hiyo ni usalama na kwamba mwenendo wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) unakwenda kinyume na misingi ya Shirika la Usalama na Ushirikiano wa Ulaya.

Sergey Naryshkin amesema shirika la kijeshi la NATO limezidisha mapigano na mivutano katika nchi mbalimbali.