Polisi 61 wa Marekani wauawa katika machafuko
Maafisa 61 usalama nchini Marekani wameuawa kwa kupigwa risasi tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi hivi sasa.
Kwa mujibu wa Press TV, takwimu zilizotolewa hivi karibuni na mfuko wa kumbukumbu za maafisa wa kulinda usalama wa taifa nchini Marekani zinaonesha kuwa, madhara waliyopata maafisa wa polisi yameongezeka kwa asilimia 48 ikilinganishwa na mwaka jana.
Sababu zilizopelekea kuongezeka chuki dhidi ya vyombo vya usalama hata ndani ya Marekani ni pamoja na ukatili unaofanywa na polisi wa Marekani dhidi ya raia na kuongezeka mauaji ya watu bila ya sababu yoyote hususan dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika na watu wengine wa jamii za wachache katika miaka ya hivi karibuni.
Mfuko wa kuwakumbuka maafisa wa kulinda usalama wa taifa wa Marekani nao umethibitisha jambo hilo na kusema ndilo liliyopelekea kuongezeka chuki dhidi ya jeshi la polisi katika pembe mbalimbali za nchi hiyo.