Kuongeza hujuma na jinai mbalimbali Marekani baada ya ushindi wa Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i20455-kuongeza_hujuma_na_jinai_mbalimbali_marekani_baada_ya_ushindi_wa_trump
Kundi moja la Kutetea Haki za Kiraia nchini Marekani limesema katika ripoti yake kuwa, hujuma na jinai mbalimbali ziliongezeka nchini humo humo siku kumi baada ya Donald Trump kutangazwa mshindi wa kiti cha urais.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Nov 30, 2016 01:00 UTC
  • Kuongeza hujuma na jinai mbalimbali Marekani baada ya ushindi wa Trump

Kundi moja la Kutetea Haki za Kiraia nchini Marekani limesema katika ripoti yake kuwa, hujuma na jinai mbalimbali ziliongezeka nchini humo humo siku kumi baada ya Donald Trump kutangazwa mshindi wa kiti cha urais.

Takwimu hizo zilizotolewa na Taasisi kwa jina la Southern Poverty Law Center zimebainisha kuwa katika muda wa siku kumi baada ya Donald Trump kutangazwa mshindi wa kiti cha Urais, kulitokea mashambulizi ya chuki 867 huko Marekani;  ambapo miongoni mwa hujuma hizo tunaweza kuashiria uandikaji wa maandishi ya nara na shaari za chuki na vinyongo juu ya kuta za majengo na nyumba mbalimbali nchini humo. Richard Cohen Mkurugenzi wa kituo hicho amesema kuwa takwimu hizo zinaonyesha kuongeza pakubwa matukio yanayotokana na chuki kulinganisha na kiwango cha kawaida ambacho kimekuwa kikishuhudiwa huko Marekani.  Donald Trump Rais Mteule wa Marekani aliwahi kusema katika kampeni zake za uchaguzi kwamba, ana mpango wa kujenga ukuta mrefu katika mpaka wa nchi hiyo na nchi ya Mexico na kwa utaratibu huo, kuzuia wahajiri haramu kuingia Marekani.

Rais Mteule wa Marekani Donald Trump