Marekani wanachunguza kurasa za Facebook za wasafiri
https://parstoday.ir/sw/news/world-i24439-marekani_wanachunguza_kurasa_za_facebook_za_wasafiri
Maafisa wa idara ya uhamiaji nchini Marekani wanachunguza kursa za kijamii na hasa Facebook ya wasafiri ili kubaini misimamo yao ya kisiasa.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Jan 30, 2017 01:11 UTC
  • Marekani wanachunguza kurasa za Facebook za wasafiri

Maafisa wa idara ya uhamiaji nchini Marekani wanachunguza kursa za kijamii na hasa Facebook ya wasafiri ili kubaini misimamo yao ya kisiasa.

Kwa mujibu wa gazeti la Independent, wakili  wa masuala ya uhamiaji Mana Yegani aliyeko  mjini Houston, amesema wasafiri kadhaa wenye kadi ya 'Green Card' ambayo inawapa ruhusua ya kuishi na kufanya kazi Marekani, wamesimamishwa na maafisa wa uhamiaji katika viwanja wa ndege Marekani na kusailiwa kwa masaa kadhaa baada ya  Rais Donald Trump kutia saini sheria ya kuwazuia raia wa nchi saba za Kiislamu kuingia nchini humo. Amesema maafisa wa usalama katika mipaka ya Marekani wanachunguza kurasa za Facebook za wasafiri kubaini mitazamo yao ya kisiasa kabla ya kuwaruhusu kuingia nchini humo.

Marufuku hiyo iliyotiwa saini na Trump inawahusu watu wenye pasipoti za  Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen. Hata raia wa nchi hizo walio na 'Green Card' pia wamepigwa marufuku kuingia Marekani.

Hatua hiyo ya kibaguzi ya Trump imeendelea kulaaniwa na kukosolewa katika kila kona ya dunia.