Wamarekani walio wengi wapinga marufuku ya Waislamu kuingia nchini humo
Uchunguzi mpya wa maoni uliofanyika nchini Marekani unaonesha kuwa asilimia kubwa ya raia wa nchi hiyo wanapinga marufuku ya kuingia Waislamu nchini Marekani.
Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni yanaonesha kuwa, asilimia 65 ya raia wa Marekani wanapinga marufuku ya Waislamu kuingia nchini humo na asilimia 26 pekee ndio wanaounga mkono utekelezaji wa mpango huo.
Marekani ni miongoni mwa nchi ambazo zimeasisiwa na wahajiri; na tofauti na nchi nyingine zenye ustaarabu wa kihistoria, nchi hiyo iliundwa na wahamiaji kutoka Ulaya waliohamia huko kwa sababu za kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii.
Kwa kutilia maanani ukweli huo wataalamu wanasema hatua ya serikali ya sasa ya kuwapiga marufuku Waislamu na jamii nyingine za waliowachache kuingia nchini humo haioani na historia ya jamii ya Marekani.
Tarehe 27 Januari Rais Donald Trump wa Marekani aliamuru kupingwa marufuku raia kutoka nchi 7 Kiislamu kuingia nchini humo, suala ambalo limezusha upinzani mkubwa ndani na nje ya Marekani. Uamuzi huo wa Trump pia umepingwa na kutenguliwa na mahakama za nchi hiyo.