EU yarefusha vikwazo dhidi ya Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i26350-eu_yarefusha_vikwazo_dhidi_ya_russia
Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa umerefusha vikwazo vilivyowekwa na umoja huo kwa shakhsia na mashirika ya Russia na eneo la Crimea kwa muda wa miezi sita yaani hadi kufikia Septemba 15.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 14, 2017 01:00 UTC
  • EU yarefusha vikwazo dhidi ya Russia

Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa umerefusha vikwazo vilivyowekwa na umoja huo kwa shakhsia na mashirika ya Russia na eneo la Crimea kwa muda wa miezi sita yaani hadi kufikia Septemba 15.

Umoja wa Ulaya jana Jumatatu ulitangaza kuwa, umeongeza kwa muda wa miezi mingine sita zuio la fedha na marufuku ya safari waliyowekewa raia 150 wa Russia kufuatia mgogoro ulioiathiri Ukraine mwaka 2014. Umoja wa Ulaya unawatuhumu shakhsia na mashirika hayo kuwa kuhatrisha suala la kujitawala na umoja wa ardhi ya Ukraine.

Vifaru vikipiga doria huko Crimea baada ya kuzuka mgogoro mwaka 2014

Washauri wa Rais Vladimir Putin wa Russia, wabunge, maafisa wa ulinzi na usalama, maafisa wa kijeshi na wapinzani wa mashariki mwa Ukraine wamo katika orodha ya shakhsia walioguswa na vikwazo hivyo vya Umoja wa Ulaya. Orodha ya sasa ya Umoja wa Ulaya ina jumla ya majina ya watu 150 na mashirika 37 kwa kuzingatia kufutwa majina ya watu wawili ambao wameaga dunia.

Vikwazo hivyo vinajumuisha marufuku ya kuingia katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya shakhsia hao waliotajwa pamoja na kuzuia fedha zao.