Brazil yalaani ujenzi mpya wa nyumba za Mayahudi Ukingo wa Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i27322-brazil_yalaani_ujenzi_mpya_wa_nyumba_za_mayahudi_ukingo_wa_magharibi
Brazil imelaani uamuzi uliopasishwa hivi karibuni na baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuidhinisha ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 05, 2017 07:47 UTC
  • Brazil yalaani ujenzi mpya wa nyumba za Mayahudi Ukingo wa Magharibi

Brazil imelaani uamuzi uliopasishwa hivi karibuni na baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuidhinisha ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Brazil imesema kuwa, upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu mbali na kuwa ni kinyume cha sheria za kimataifa, lakini pia unazidi kuvuruga kile kinachotajwa kama mchakato wa kuundwa nchi mbili ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa zaidi ya karne tano wa Palestina na Israel.

Wizara hiyo imekariri msimamo wa serikali ya Brasilia wa kutaka kuudwa taifa huru la Palestina kwa misingi ya michoro ya mipaka ya mwaka 1967.

Haya yanajiria siku chache baada ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri kutoa taarifa kama hiyo na kulaani hatua ya utawala wa Kizayuni ya kuidhinisha ujenzi wa nyumba mpya za walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Bendera za Brazil na Palestina

Kadhalika hivi karibuni, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ilitoa taarifa na kusema kuwa, siasa za ujenzi na upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi ya Palestina ni ukiukaji wa haki za taifa la Palestina.

Hii ni katika hali ambayo, Michael Lynk, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu huko Palestina amesema kuwa, jamii ya kimataifa ina wajibu wa kuchukua hatua nyingi zaidi mbali ya maazimio na kutoa taarifa tu ili kukomesha kukaliwa kwa mabavu Palestina na ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina.