Kremlin: Lengo la Russia ni kupambana na magaidi Syria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i27692-kremlin_lengo_la_russia_ni_kupambana_na_magaidi_syria
Msemaji wa ikulu ya Russia (Kremlin) amesema kuwa lengo la nchi hiyo ni kuendesha mapambano dhidi ya magaidi huko Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 12, 2017 22:56 UTC
  • Kremlin: Lengo la Russia ni kupambana na magaidi Syria

Msemaji wa ikulu ya Russia (Kremlin) amesema kuwa lengo la nchi hiyo ni kuendesha mapambano dhidi ya magaidi huko Syria.

Dmitry Peskov amesema suala la kuitaka Moscow kusitisha uungaji mkono wake kwa Damascus ni sawa na kuombwa na magaidi kutekeleza mashambulizi dhidi ya serikali halali ya Syria. Msemaji wa Kremlin ameongeza kuwa baadhi ya pande zinajaribu kueneza taarifa za uwongo kuhusu Russia na kuituhumu nchi hiyo kwa kutoa madai ya kutekelezwa shambulio la kemikali katika eneo la Khan Sheikhoun kusini mwa mji wa Idlib huko Syria.

Wahanga wa shambulio la kemikali huko Khan Shaykhun Syria 

 Dmitry Peskov ameongeza kuwa Moscow huko Syria inatafuta njia ya kutatua mgogoro wa nchi hiyo kwa njia za kidiplomasia bila ya kutumia nguvu za kijeshi na kukabiliana na kundi la Daesh. Weledi wengi wa mambo wanakitaja  kitendo cha kuituhumu serikali ya Syria kuwa imetumia silaha za kemikali kuwa ni katika juhudi za kuzipotosha fikra za waliowengi na kuficha uhakika wa mambo kufuatia ushindi wa hivi karibuni wa jeshi la Syria mbele ya magaidi nchini humo.