Kuhani mmoja Mzayuni atimuliwa Russia
Idara ya Mahakama ya Russia imemfukuza nchini humo kuhani mmoja Mzayuni aliyekuwa akifanya harakati za siri na kuendesha kituo maalumu cha misaada bila ya idhini ya nchi hiyo.
Shirika la habari la Ufaransa limeripoti habari hiyo kutokea mjini Moscow na kuongeza kuwa, mahakama moja mjini humo, jana ilisikiliza kesi ya Joseph Khersonsky, kuhani Mzayuni kutoka Israel ambaye amekuwa akiishi nchini Russia kwa muda wa miaka 10 sasa. Mahakama hiyo imempiga faini ya Euro 80 elfu kuhani huyo Mzayuni na kumfukuza nchini Russia. Idara ya Mahakama ya Russia imempata na hatia kuhani huyo, ya kuanzisha kituo cha kigeni cha misaada, bila ya idhini ya nchi hiyo.
Miezi mitatu iliyopita pia, Idara ya Mahakama ya Russia ilimtimua nchini humo kuhani mmoja Mzayuni raia wa Marekani kutokana na kuhatarisha usalama wa taifa hilo.
Kuhani huyo alikuwa mkuu wa Mayahudi katika mji wa Sochi wa kusini magharibi mwa Russia tangu mwaka 2002 na alitimuliwa nchini humo miezi mitatu iliyopita baada ya kupatikana na hatia ya kuhatarisha usalama wa Russia. Kuhani huyo alifukuzwa Russia, yeye na familia yake.
Utawala wa Kizayuni wa Israel ni maarufu kwa kufanya ujasusi, kuhatarisha usalama wa mataifa mengine, kuiba nyaraka za siri na kuingilia mambo ya ndani ya nchi hizo kwa njia tofauti.