Ubaguzi dhidi ya wafungwa weusi waongezeka Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i32208-ubaguzi_dhidi_ya_wafungwa_weusi_waongezeka_marekani
Uchunguzi mpya umebaini kuwa, ubaguzi wa kimbari dhidi ya wafungwa weusi wenye asili ya Afrika umeongezeka nchini Marekani.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Jul 24, 2017 15:01 UTC
  • Ubaguzi dhidi ya wafungwa weusi waongezeka Marekani

Uchunguzi mpya umebaini kuwa, ubaguzi wa kimbari dhidi ya wafungwa weusi wenye asili ya Afrika umeongezeka nchini Marekani.

Jarida la kila wiki la Newsweek limeripoti kuwa, matokeo ya uchunguzi uliofanywa hivi karibuni na taasisi ya Urban Institute yenye makao yake mjini Washington unaonesha kuwa, kiwango cha hukumu za kufungwa jala Wamarekani weusi kimeongeza sana nchini humo. 

Matokeo ya uchunguzi huo yanasema kuwa, wanaume weusi ndio wanaounda sehemu kubwa ya wafungwa waliohukumiwa vifungo vya muda mrefu nchini Marekani. Uchunguzi huo umebaini kuwa, Wamarekani weusi ndiyo wanaounda sehemu kubwa zaidi ya wafungwa waliohukumiwa vifungo vya miaka mingi katika majimbo 35 yaliyohusisha uchunguzi huo. 

Katika jimbo la Pennsylvania peke yake Wamarekani weusi wanaunda asilimia 49 ya wafungwa wote lakini asilimia 60 ya wafungwa waliohukumiwa vifungo vya muda mrefu zaidi ni Wamarekani wenye asili ya Afrika.  

Katika miaka ya hivi karibuni pia kumetolewa ripoti nyingi zinazolaani ukatili na ubaguzi wa polisi ya Marekani dhidi ya raia wesi wa nchi hiyo.