Matamshi ya chuki ya Netanyahu dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i33592-matamshi_ya_chuki_ya_netanyahu_dhidi_ya_iran
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mara nyingine ameonana na Rais Vladimir Putin wa Russia katika mji wa Sochi na kujaribu kwa tamaa zake kuionesha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa eti ni nchi hatari katika eneo la Mashariki ya Kati na duniani kiujumla; hata hivyo amefeli.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 25, 2017 02:05 UTC
  • Benjamin Netanyahu (kushoto) katika mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Russia
    Benjamin Netanyahu (kushoto) katika mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Russia

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mara nyingine ameonana na Rais Vladimir Putin wa Russia katika mji wa Sochi na kujaribu kwa tamaa zake kuionesha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa eti ni nchi hatari katika eneo la Mashariki ya Kati na duniani kiujumla; hata hivyo amefeli.

Mazungumzo ya wawili hao yalifanyika Jumatano jioni, na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni alifanya juhudi kubwa za kumshawishi Putin akubaliane na siasa za Israel za kuonesha kuwa ushawishi wa Iran katika nchi Syria, Yemen na Lebanon ni hatari kubwa. Hata hivyo Rais wa Russia hakutia neno lake isipokuwa kumsikiliza tu waziri mkuu huyo wa Israel. Baada ya Netanyahu kukariri madai yake yasiyo na msingi dhidi ya Iran kama kudai kuwa eti Tehran ina mchango hasi nchini Syria, mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amejibu madai hayo ya Israel na kupinga vikali madai hayo ya Netanyahu. Vasily Nebenzya, mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amezungumza na waandishi wa habari kuhusu mazungumzo ya Netanyahu na Putin pamoja na madai yaliyotolewa na Israel dhidi ya Iran. Amesema: Tehran inatoa mchango mzuri katika juhudi za kutatua mgogoro wa Syria na inashirikiana vizuri na kwa karibu na Moscow katika jambo hilo

Magaidi wanaosaidiwa na madola ya kibeberu kufanya jinai katika nchi za Kiislamu hasa Syria na Iraq

 

Hatua ya Benjamin Netanyahu ya kuhakikisha anaonana tena na Rais wa Russia ni aina fulani ya kugawana kazi Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kutekeleza njama za kila namna za kuishinikiza zaidi Tehran kwa tamaa ya kufanikisha ndoto zao za kuifanya Iran ionekane ni nchi inayozusha migogoro. Siku hiyo hiyo ya Jumatano, Nikki Haley, mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa alionana na Yukia Amano, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki mjini Vienna kwa shabaha ya kushadidisha mashinikizo dhidi ya Iran kupitia makubaliano ya nyuklia ya JCPOA. Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, kusadifiana mazungumzo hayo ya mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA mjini Vienna na mazungumzo ya Waziri Mkuu wa Israel na Rais wa Russia mjini Sochi huku Iran ikiwa ajenda kuu ya Nikki Haley na Netanyahu katika mazungumzo yote hayo mawili, si jambo lililotokea kwa sadfa, bali ni kitu kilichopangwa tangu zamani.

Njama zinazofanywa kwa pamoja na Marekani na Israel za kuituhumu Iran kuwa eti ni nchi inayosababisha migogoro, zinafanyika katika hali ambayo ushirikiano wa kiistratijia kati ya Iran na Russia nchini Syria umebadilisha milingano ya kisiasa na ya medani za vita nchini humo na kusambaratisha njama za Israel na Marekani ambazo zinayatumia magenge ya kigaidi kuzusha migogoro na kuhatarisha usalama wa eneo hili zima. Ubunifu uliofanywa na Iran, Russia na Uturuki wa kusimamia mazungumzo ya amani ya Syria ya Astana na kufanikiwa kuyafanya maeneo manne ya Syria kutokuwa na vita umewakasirisha sana maadui wa ulimwengu wa Kiislamu hususan Israel na Marekani. Ushirikiano huo wa kiistratijia wa Iran na Russia umeyasambaratisha magenge ya kigaidi katika kona mbalimbali za Syria na wakati huo huo kukaribia kutatuliwa mgogoro wa miaka mingi sasa wa nchi hiyo ya Kiarabu. Yote hayo yanaonesha mchango chanya na muhimu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika vita vya kweli vya kupambana na ugaidi na katika utatuzi wa mgogoro wa miaka saba sasa wa Syria. 

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akimpa mkono gaidi aliyejeruhiwa katika vita nchini Syria. Israel inawatibu magaidi hao ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

 

Ni jambo lililo wazi kuwa mafanikio hayo hayawafurahishi hata kidogo maadui wa Syria hususan Israel na Marekani. Si hayo tu, lakini pia utawala wa Kizayuni wa Israel ndio unaokwamisha juhudi za kutatua mgogoro wa Syria. Jenerali Amir Eshel, mkuu wa zamani wa kikosi cha anga ya Israel alikiri wiki iliyopita kwamba, ndege za utawala wa Kizayuni zimefanya mashambulizi karibu mia moja ndani ya ardhi ya Syria katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.  

Mashambulizi ya mara kwa mara ya anga na makombora yanayofanywa na Israel dhidi ya Syria sambamba na utawala wa Kizayuni kuwasaidia waziwazi magaidi wanaofanya jinai ndani ya ardhi ya Syria ikiwa ni pamoja na kuwatibu majeraha yao katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, ni ushahidi wa wazi kuwa madola ya kibeberu kama Israel na Marekani ndio wakwamishaji wakuu wa jitihada za kuutatua kikamilifu mgogoro wa Syria. Uchokozi wa utawala wa Kizayuni ndani ya ardhi ya Syria ni mkubwa sana kiasi kamba mwezi Aprili mwaka huu, Russia ilimwita balozi wa Israel mjini Moscow, Gary Koren, kulalamikia mashambulizi ya anga ya ndege za Israel karibu na maeneo waliko wanajeshi wa Russia nchini Syria. Ikumbukwe kuwa, tofauti kabisa na madola vamizi, nchi kama Russia imetuma wanajeshi wake huko Syria kwa ombi rasmi la serikali iliyochaguliwa na wananchi wenyewe wa Syria.

Shambulio la Israel katika ardhi ya Syria