EU yasisitizia haja ya kuheshimiwa makubaliano ya JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/world-i33760-eu_yasisitizia_haja_ya_kuheshimiwa_makubaliano_ya_jcpoa
Kwa mara nyingine tena Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefungamana na ahadi zake kuhusiana na makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa baina yake na kundi la 5+1 yanayofahamika kama JCPOA na kusisitizia udharura wa kuheshimiwa hati hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 29, 2017 02:58 UTC
  • EU yasisitizia haja ya kuheshimiwa makubaliano ya JCPOA

Kwa mara nyingine tena Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefungamana na ahadi zake kuhusiana na makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa baina yake na kundi la 5+1 yanayofahamika kama JCPOA na kusisitizia udharura wa kuheshimiwa hati hiyo.

Federica Mogherini amesema hayo katika kikao cha wazi cha Kongamano la Mabalozi wa Umoja wa Ulaya cha jana Jumatatu mjini Brussels na kuongeza kuwa, makubaliano hayo yanaashiria 'msimamo halisi wa Ulaya katika sera za kigeni.'

Mogherini amesisitiza kuwa: "Nimekariri mara kwa mara kuwa, huu sio mkataba wa nchi mbili, ni makubaliano ya kimataifa yaliyofikiwa na pande kadhaa." 

Baadhi ya viongozi waliosaini JCPOA

Matamshi ya Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya yameonekana kwa njia isiyo ya moja kwa moja kukosoa msimamo wa Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye amekuwa akisisitiza kuwa, makubaliano ya JCPOA ndio muafaka mbaya zaidi kutiwa saini na serikali ya Washington katika miaka ya hivi karibuni.

Mogherini ameongeza kuwa, makubaliano hayo yaliyofikiwa Julai mwaka 2015 huko mjini Veinna na kuanza kutekelezwa rasmi Januari mwaka jana 2016, ni muafaka uliopata baraka za jamii ya kimataifa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, na pande zote husika zinafaa kuuunga mkono na kuutekeleza kikamilifu.