Idadi ya Waislamu wa Rohingya wanaokimbilia Bangladesh inazidi kuongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/world-i33934-idadi_ya_waislamu_wa_rohingya_wanaokimbilia_bangladesh_inazidi_kuongezeka
Kufuatia kuendelea operesheni za jeshi la serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu wa kabila la Rohingya katika jimbo la Rakhine, idadi kubwa ya Waislamu wa eneo hilo wameendelea kukimbia ili kuokoa maisha yao.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 05, 2017 02:36 UTC
  • Idadi ya Waislamu wa Rohingya wanaokimbilia Bangladesh inazidi kuongezeka

Kufuatia kuendelea operesheni za jeshi la serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu wa kabila la Rohingya katika jimbo la Rakhine, idadi kubwa ya Waislamu wa eneo hilo wameendelea kukimbia ili kuokoa maisha yao.

Mashirika ya misaada ya kibinaadamu nchini Bangladesh yametahadharisha kutokana na hali mbaya iliyopo katika kambi za wakimbizi walipowekwa Waislamu wa Rohingya katika mpaka wa pamoja kati ya Myanmar na Bangladesh. Kwa mujibu wa mashirika hayo, kambi hizo zimefurika idadi ya wakimbizi hao na kwamba hazina uwezo wa kuendelea kupokea Waislamu wengine.

Hujuma na ukatili wa jeshi la Myanmar dhidi ya makazi ya Waislamu

Shirini Arifai, mwandishi wa habari wa televisheni ya Press TV ameripoti kuhusiana na habari hiyo kwamba, kuendelea ukandamizaji na ukatili wa kupindukia dhidi ya Waislamu wa Rohingya katika jimbo la Rakhine, ndani ya kipindi cha siku 10 zilizopita, kumewafanya karibu Waislamu 75 elfu kukimbilia nchini Bangladesh na sasa watu hao wanahitaji msaada wa dharura ili kuokoa maisha yao. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baadhi ya Waislamu hao waliofanikiwa kufika katika mpaka huo wa pamoja wanakutwa wakiwa na majeraha makubwa ya kupigwa risasi na kadhalika, huku wengine wakipatwa na matatizo ya kisaikolojia kutokana na kushuhudia mauaji ya kutisha ya askari wa serikali na Mabudha dhidi ya ndugu na jamaa zao.

Mabudha makatili wanaohusika na mauaji dhidi ya Waislamu wanaodhulumiwa

Mwandishi huyo wa habari wa kanali ya Press TV ameongeza kuwa, aghlabu ya wakimbizi hao Waislamu wanaamini kuwa, mashinikizo pekee ya ulimwengu wa Kiislamu na kadhalika sisitizo la nchi tofauti dhidi ya serikali ya Myanmar, ndio vitaweza kukomesha wimbi la mauaji na ukatili wa nusu karne dhidi ya raia madhlum wa Rohingya nchini Burma. Tangu tarehe 25 Agosti mwaka huu, jeshi la Myanmar kwa kushirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali limekuwa likiwashambulia kwa namna ya kutisha Waislamu wa jimbo la Rakhine wasio na ulinzi.