Wamarekani waandamana kuupinga utawala wa Kizayuni wa Israel
Idadi kubwa ya Mayahudi ambao ni wafuasi wa Kanisa la Orthodox pamoja na wanaharakati wa Kipalestina wameandamana nchini Marekani na kukusanyika mbele ya Ikulu ya White House wakiulaani utawala haramu wa Israel unaotenda jina kila leo dhidi ya Wapalestina.
Washiriki wa maandamano hayo wametoa wito wa kuhitimishwa mara moja uwepo wa Israel na kurejeshewa Wapalestina ardhi zilizoghusubiwa na utawala huo ghasibu.
Waandamanaji hao walikusanyika mbele ya ikulu ya Marekani White House na kupiga nara dhidi ya utawala vamizi wa Israel na kutoa wito wa kuhitimishwa ukaliaji mabavu wa ardhi za Wapalestina.
Katika maandamano mengine yaliyofanyika Washington DC, wanaharakati walioshiriki maandamano hayo walikusanyika mbele ya mahala panapofanyika mkutano wa kila mwaka wa lobi za Wazayuni ambazo ni wafuasi wa Israel na kupiga nara wakiulaani utawala huo ghasibu pamoja na waungaji mkono wake.
Maandamano hayo ni mwenendelezo wa mashinikizo ya jamii ya kimataifa dhidi ya utawala ghasibu wa Israel ambao umekuwa ukitenda jinai kila leo dhidi ya wananchi madhlumu wa Wapalestina.
Kushadidi mashikizo ya kila upande dhidi ya Israel ni ishara ya kuongezeka harakati zilizo dhidi ya Israel kutokana na vitendo vyake visivyo vya kibinadamu dhidi ya wananchi wa Palestina.