Wayahudi wa Marekani wapinga vikali siasa za serikali ya Trump
Mayahudi nchini Marekani wamepinga vikali siasa za serikali ya nchi hiyo kuhusu makubaliano ya JCPOA yaliyofikiwa kati ya Iran na kundi la 5+1.
Matokeo ya uchunguzi wa maoni ulioendeshwa na taasisi kwa jina la "Institute for Social Science Research Solutions" iliyotumwa kazi hiyo na Jumuiya ya Kuwaunga Mkono Mayahudi duniani yameonyesha kuwa asilimia 68 ya Mayahudi wa Marekani hawaungi mkono siasa za serikali ya Rais Trump bali ni asilimia 26 tu ndio wanaounga mkono siasa hizo.
Uchunguzi huo wa maoni ulifanywa kuanzia tarehe 10 hadi 28 Agosti mwaka huu. Jamii ya Mayahudi wa Marekani wanapinga sera za serikali ya Trump kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran licha ya serikali ya Trump kukosoa waziwazi na nyuma ya pazia makubaliano hayo ya JCPOA.
Msimamo na siasa hizo za ikulu ya Marekani (White House) zinadhihirisha namna Marekani ilivyoshindwa kutekeleza masuulia na majukumu yake kuhusu moja ya makubaliano muhimu ya pande kadhaa yaliyofikiwa katika miaka ya hivi karibuni baada ya kupita miaka miwili ya kutekelezwa kati ya Iran na madola makuu duniani na licha ya Jamhuri ya Kiislamu kuthibitisha kwa mara kadhaa kuheshimu na kutekeleza majukumu yake mkabala na makubaliano hayo.