ICC yatahadharisha kuhusu uhalifu dhidi ya wahamiaji Libya
https://parstoday.ir/sw/news/world-i36267-icc_yatahadharisha_kuhusu_uhalifu_dhidi_ya_wahamiaji_libya
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, imeonya kuwa itachukua hatua kuhusu wanaotenda uhalifu dhidi ya wahamiaji waliofungwa au kusafirishwa kwa njia haramu kupitia Libya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 09, 2017 00:45 UTC
  • Fatou Bensouda
    Fatou Bensouda

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, imeonya kuwa itachukua hatua kuhusu wanaotenda uhalifu dhidi ya wahamiaji waliofungwa au kusafirishwa kwa njia haramu kupitia Libya.

Kauli hiyo imetolewa na mwendesha mashtaka wa ICC, Bi Fatou Bensouda, akihutubia kikao cha Baraza la Usalama kilichokutana Jumatano kujadili hali nchini Libya.

Bensouda amesema iwapo ukatili mkubwa utaendelea kutekelezwa ,hata sita kutoa tangazo la kukamatwa kwa wahalifu wanaotekeleza vitendo hiyvo.

Ameongeza kwamba ICC inaendelea kusikitishwa na uhalifu unaotekelezwa dhidi ya wahamiaji walio hatarini wakitumia Libya kama njia ya kufika Ulaya kupitia njia ya bahari huku wengi wakiendelea kushikiliwa katika vituo na wengine kufa jangwani.

Wahajiri haramu wakiwa katika pwani ya Libya

Kwa mantiki hiyo amesema ofisi yake itaendelea kutathmini ukatili unaotekelezwa dhidi ya wahamiaji wanaopitia Libya.

Siasa za kupenda vita za nchi za Magharibi katika eneo la Mashariki ya Kati na katika baadhi ya nchi za Afrika zimewalazimisha mamilioni ya watu kukimbia nchi zao zilizovamiwa na machafuko na kutafuta usalama wa roho zao katika nchi nyingine.