Mvutano katika uhusiano wa Misri na Uturuki
(last modified Wed, 07 Feb 2018 14:49:56 GMT )
Feb 07, 2018 14:49 UTC
  • Mvutano katika uhusiano wa Misri na Uturuki

Uhusiano wa Misri na Uturuki umeharibika kuhusiana na suala la uchoraji mipaka katika Bahari ya Mediterania.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Irna, Ahmad Abu Zeid, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema kuwa Mapatano ya nchi hiyo na Cyprus kuhusiana na uchoraji wa mipaka ya majini katika Bahari ya Maditerania ni ya kisheria na kwamba Misri itakabiliana na juhudi zozote za kukiuka utawala na mamlaka yake juu ya eneo la kiuchumi mashariki mwa bahari hiyo. Ameongeza kuwa maafikiano ya kuchora mipaka ya baharini baina ya Misri na Cyprus ni mkataba wa kimataifa ambao imesajiliwa katika Umoja wa Mataifa.

Bahari ya Mediterania

Mevlüt Çavuşoğlu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki alisema siku ya Jumatatu kwamba nchi hiyo haitambui rasmi mkataba wa kuainisha mipaka ya baharini uliotiwa saini kati ya Misri na Cyprus mwaka 2013 kwa ajili ya kunufaika kiuchumi na maliasili ya eneo hilo. Uhusiano wa Misri na Uturuki umekuwa na mvutano tokea wakati wa kung'olewa madarakani Muhammad Mursi wa Misri mwaka 2013.

Tags