Korea Kaskazini: Tuhuma bandia za Marekani dhidi yetu zitaigharimu Washington
https://parstoday.ir/sw/news/world-i40439-korea_kaskazini_tuhuma_bandia_za_marekani_dhidi_yetu_zitaigharimu_washington
Serikali ya Korea Kaskazini imetangaza kwamba, kitendo cha Marekani kuendeleza mashinikizo dhidi yake, kitaigharimu Washington.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 16, 2018 07:34 UTC
  • Korea Kaskazini: Tuhuma bandia za Marekani dhidi yetu zitaigharimu Washington

Serikali ya Korea Kaskazini imetangaza kwamba, kitendo cha Marekani kuendeleza mashinikizo dhidi yake, kitaigharimu Washington.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini ikijibu vitisho mtawalia vya Marekani dhidi ya nchi hiyo imesema kuwa, tabia ya Washington ya kutoa tuhuma dhidi ya Pyongyang kwamba inakiuka haki za binadamu, zitaigharimu Marekani yenyewe.

Otto Frederick Warmbier, kijana Mmarekani enzi za uhai wake akiwa chini ya ulinzi Korea Kaskazini

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini, Washington inafanya njama mbalimbali za kuchafua sura ya nchi hiyo ya Asia kwa walimwengu kwa kutumia kisingizio cha haki za binadamu.

Kabla ya hapo kijana mmoja raia wa Marekani kwa jina la Otto Frederick Warmbier alikamatwa na serikali ya Korea Kaskazini kwa tuhuma za ujasusi. Hata hivyo baada ya kuachiliwa kwake na kurejea nchini Marekani, alifariki dunia. Kufuatia tukio hilo Washington iliitaja Pyongyang kwamba ndio iliyohusika na kifo cha Otto Warmbier sambamba na kuanzisha kampeni kubwa za kuituhumu Korea Kaskazini kuwa inakiuka haki za binadamu.

Miradi ya nyuklia ya Korea Kaskazini inayoitia kiwewe Marekani na Japan

Wakati huo huo, Chou Riong Haye mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa chama tawala nchini Korea Kaskazini amesema kuwa, Pyongyang ina mpango wa kuimarisha na kukamilisha miradi yake ya silaha za nyuklia. Hii ni katika hali ambayo Shinzō Abe, Waziri Mkuu wa Japan na Rais Donald Trump wa Marekani hivi karibuni walifanya mazungumzo kwa njia ya simu wakitaka kushadidishwa mashinikizo na vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini kwa kile walichokisema kuwa ni kuipokonya nchi hiyo silaha zake za nyuklia.