Trump aunga mkono tena sheria ya kumiliki bunduki kiholela nchini Marekani
Kwa mara nyingine tena rais wa Marekani, Donald Trump ameunga mkono sheria inayoruhusu kuuzwa na kumiliki bunduki kiholela nchini humo.
Shirika la habari la IRIB limeripoti habari hiyo na kusema kuwa, licha ya kuweko upinzani mkali dhidi ya sheria hiyo ya kubeba bunduki hasa baada ya mashambulizi holela ya silaha kushadidi nchini Marekani, lakini Donald Trump ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuunga mkono waziwazi sheria hiyo.
Katika ujumbe wake kupitia Twitter, Trump amesema kuwa, kipengee cha pili cha katiba (kinachohusiana na kuruhusu na kuunga mkono sheria ya kubeba bunduki) kitapasishwa tu licha ya Wademocrat na baadhi ya viongozi wa nchi hiyo kupinga sheria hiyo.
Hii ni katika hali ambayo kila mwaka maelfu ya watu wanauawa na kujeruhiwa nchini Marekani kutokana na mashambulizi ya kiholela ya silaha.
Wamiliki wa mashirika makubwa ya kutengeneza silaha nchini Marekani wengi wao ni Wazayuni na wana ushawishi mkubwa katika Congress na Ikulu ya Marekani (White House), hivyo hawaruhusu kubanwa biashara ya silaha zinazozalishwa na mashirika hayo.