Maandamano yafanyika Marekani chini ya nara " Hatutaki vita Syria"
Makumi ya wananchi wa Marekani wanaopinga vita wamefanya maandamano katika miji mbalimbli ya nchi hiyo kulalamikia kushambuliwa kijeshi Syria. Wanaharakati hao wanaopinga vita wameandamana baada ya kutekelezwa mashambulizi ya makombora dhidi ya Syria chini ya uongozi wa Marekani.
Wakiwa katika miji ya Washington DC na Los Angeles, waandamanaji hao wameshuhudiwa wakipiga nara dhidi ya mashambulizi dhidi ya Syria yaliyoongozwa na Marekani kwa kushirikiana na Ufaransa na Uingereza.
Kundi la waandamanaji wanaharakti wanaopinga vita kwa jina la CODE PINK pia walikuwa wamebeba mabango yanayolaani vita hivyo visivyo vya kiakhlaqi na vilivyo kinyume cha sheria. Kundi hilo linalopinga vita aidha limefanya maandamano huko San Francisco karibu na nyumbani kwa maseneta wawili watajika wa Marekani, Nancy Pelosi kiongozi wa waliowachche wa chama cha Democrat katika bunge la wawakilishi na Seneta Dianne Feinstein ambao wote wanaliwakilisha eneo la San Francisco. Wafanya maandamano hao walikuwa wamebeba pia bendera za Syria katika maandamano yao huko San Francisco. Wafanya maandamano wengine katika mji wa Chicago pia walipiga shaari huku wakiwa wamebeba mabango wanayolaani mashambulio ya makombora ya serikali ya Marekani huko Syria.
Wafanya maandamano wamebainisha kutiwa shaka na lengo halisi la Marekani la kutekeleza mashambulio hayo ya kijeshi huko Syria na kutangaza kuwa mashambulizi hayo hayakutekelezwa kwa lengo la kuwalinda raia. Itakumbukwa kuwa Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi Jumamosi alfajiri ziliishambulia kwa makombora Syria baada ya kushindwa magaidi huko Ghouta ya Mashariki na kufuatia nchi hizo kuibua madai ya uwongo kwamba, silaha za kemikali zimetumiwa huko Douma Syria.