Tahadhari kuhusu njama zinazofanyika dhidi ya Uislamu na Iran
Mwanafikra na kiongozi wa ngazi za juu wa kidini nchini Algeria ametahadharisha kuhusu njama zinazofanywa dhidi ya Uislamu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Khalid bin Tunisia ametahadharisha kuwa, baadhi ya wapenda vita wanafanya njama za kutoa pigo kwa Iran na Waislamu na kwamba kuna udharura wa kuwa macho na kuchukua tahadhari.
Bin Tunisia ambaye ndiye aliyetoa fikra ya "Maisha ya Amani Baina ya Watu Wote" iliopasishwa na Umoja wa Mataifa, amesifu jitihada kubwa zinazofanywa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kueneza amani na kudumisha usalama na kusema: Kizazi kijacho kinapaswa kufundishwa umuhimu wa amani na kuwa msingi wa mustakbali mwema.
Msomi huyo ametilia mkazo udharura wa kuwepo ushirikiano na kutumia teknolojia mpya kwa ajili ya kutimiza malengo ya kibinadamu kuimarisha amani, utulivu na maelewano baina ya jamii mbalimbali.
Mwaka 2017 Umoja wa Mataifa ulipasisha pendekezo lililotolewa na Algeria na kuitangaza tarehe 16 Mei kuwa ni Siku ya Kuishi kwa Amani.