Kkiwango cha watoto na vijana wanaojiua nchini Marekani kimeongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46266-kkiwango_cha_watoto_na_vijana_wanaojiua_nchini_marekani_kimeongezeka
Tovuti ya Intaneti ya New York Post imekutaja kuongezeka kiwango cha vitendo vya kujiua vijana na watoto wadogo nchini Marekani kuwa ni habari ya kuogofya kwa akina mama na akina baba.
(last modified 2025-11-09T00:45:59+00:00 )
Jun 24, 2018 14:44 UTC
  • Kkiwango cha watoto na vijana wanaojiua nchini Marekani kimeongezeka

Tovuti ya Intaneti ya New York Post imekutaja kuongezeka kiwango cha vitendo vya kujiua vijana na watoto wadogo nchini Marekani kuwa ni habari ya kuogofya kwa akina mama na akina baba.

Tovuti hiyo imeripoti kuwa utafiti uliofanywa na kisha matokeo yake kuchapishwa hivi karibuni katika makala ya afya ya watoto kwa jina la Pediatrics umeonyesha kuwa asilimia 80 ya matukio ya kulazwa hospitalini huko Marekani yanahusiana na vitendo vya kujiuwa watoto katika kipindi ambacho wapo masomoni. 

Uchunguzi huo umeendelea kubainisha kuwa baina ya kiwango hicho, asilimia 50 ya vijana waliojiuwa walikuwa na umri kati ya miaka 15 hadi 17 huku asilimia 37 ikiwa ni ya watoto walio na umri wa miaka kuanzia 12 hadi 14.

Dakta Greg Plemenz anasema kuwa uzito wa masomo na utumiaji wa mitandao ya kijamii ni kati ya sababu zinazowapelekea vijana na watoto kuamua kujiuwa.