Umoja wa Ulaya wasisitiza kulinda mapatano ya nyuklia ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46528-umoja_wa_ulaya_wasisitiza_kulinda_mapatano_ya_nyuklia_ya_iran
Mkuu wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya amesisitzia kuwa umoja huo unataka mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana rasmi kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji,JCPOA, yatekelezwe kikamilifu.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Jul 03, 2018 00:08 UTC
  • Umoja wa Ulaya wasisitiza kulinda mapatano ya nyuklia ya Iran

Mkuu wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya amesisitzia kuwa umoja huo unataka mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana rasmi kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji,JCPOA, yatekelezwe kikamilifu.

Kwa mujibu wa Maya Kosyanchych, msemaji wa Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, akizungumza na waandishi habari Jumatatu amesema: 'Umoja wa Ulaya unafungamana na utekelezwaji kikamilifu na wenye taathira wa mapatano ya nyuklia ya Iran. Hii ni kwa sababu  JCPOA ni kwa maslahi ya usalama wa Ulaya na jamii ya kimataifa.

Maya Kosyanchych ameongeza kuwa, Umoja wa Ulaya na washirika wake wa kimataifa watendelea kulinda mapatano ya JCPOA na hadi sasa wamechukua hatua za kunufaika na mapatano hayo.

Baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kutangaza mnamo Mei 8 kuwa nchi yake imejiondoa katika mapatano hayo ya JCPOA na kufuatia ombi la nchi za Ulaya za kutaka mapatano hayo yalindwe na yadumishwe, Iran ilizipatia nchi za Ulaya fursa ili ziweze kuwasilisha mapendekezo ya kudhamini kivitendo maslahi ya Iran katika JCPOA pale Marekani itakaporejesha vikwazo vyake.

Kwa kuzingatia historia hasi ya Umoja wa Ulaya katika kukiuka ahadi zake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alitoa masharti kadhaa kwa umoja huo katika mapatano hayo ya nyuklia. Miongoni mwa masharti hayo ni kutojadiliwa suala la makombora ya Iran, ushawishi wa Iran katika eneo la Mashariki ya Kati, EU kutakiwa kununua mafuta ya Iran kwa kiwango kinachotakiwa, kuwepo uhusiano wa kibenki kati ya Iran na Umoja wa Ulaya na umoja huo kupinga wazi vikwazo vya Marekani dhidi ya taifa hili.