Interpol yatahadharisha, Daesh watafanya tena mashambulizi Ulaya
https://parstoday.ir/sw/news/world-i50309-interpol_yatahadharisha_daesh_watafanya_tena_mashambulizi_ulaya
Katibu Mkuu wa Polisi ya Kimataifa (Interpol) ametahadharisha kuhusu uwezekano wa kundi la kigaidi la Daesh kufanya tena mashambulizi katika nchi za Ulaya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 21, 2018 00:23 UTC
  • Interpol yatahadharisha, Daesh watafanya tena mashambulizi Ulaya

Katibu Mkuu wa Polisi ya Kimataifa (Interpol) ametahadharisha kuhusu uwezekano wa kundi la kigaidi la Daesh kufanya tena mashambulizi katika nchi za Ulaya.

Jürgen Stock amesema kuwa, wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh kawaida wanahukumiwa vifungo vya muda mfupi na wataachiwa huru haraka na kuanza kufanya mashambulizi ya kigaidi. 

Katibu Mkuu wa Interpol ameongeza kuwa, kwa msingi huo nchi nyingi duniani zinakabiliwa na hatari ya wimbi la pili la mashambulizi na harakati za kundi la kigaidi la Daesh. 

Maafisa wengi wa nchi za Ulaya wamekuwa wakitahadharisha kuhusu hatari ya mashambulizi mapya ya kundi la kigaidi la Daesh barani humo baada ya kundi hilo kupata kipigo cha mbwa katika nchi za Iraq na Syria.

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh

Kundi la kigaidi la Daesh lilianzishwa kwa msaada wa Saudi Arabia, Marekani na washirika wao kwa shabaha ya kuvuruga amani katika nchi za Iraq na Syria na kusimika tawala zitakazolinda maslahi ya serikali ya Washington na kulinda utawala haramu wa Israel.