China yafanyia majaribio "Mama wa Mabomu Yote"
Kampuni ya kutengeneza asilaha ya China imefanya majaribio ya mafaniko ya kombora lenye nguvu zaidi lisilo la nyuklia lililopewa jina la "Mama wa Mabomu Yote".
Ripoti zinasema kuwa, kampuni ya kutengeneza silaha ya China imetangaza kuwa, majaribio ya bomu hilo yalifanywa kwa kutumia ndege ya kivita ya H-6K katika sehemu ambayo haikutajwa nchini humo na kwamba majaribio hayo yamefanyika kwa mafanikio.
Ripoti hiyo inasema bomu hilo kubwa lenye uzito wa tani kadhaa linaweza kuharibu na kubomoa kirahisi majengo ya zege, mahandaki ya chini ya ardhi na maeneo imara ya kijeshi.
Majaribio hayo ya Mama wa Mabomu Yote ya China yamefanyika huku Rais Xi Jinping wa nchi hiyo akilitaka jeshi kujitayarisha kukabiliana na mashambulizi yoyote ya nchi ambayo hakuitaja kwa jina.
Jinping ameashiria hali ya sasa ya nchi hiyo na kulitaka Jeshi la China kujitayarisha kwa ajili ya vita kwa sababu nchi inakabiliwa na hatari na changamoto zisizo na kifani.
China imekuwa ikisuguana sana na Marekani katika miaka miwili ya hivi karibuni baada ya Rais Donald Trump kushikama madaraka nchini humo.