ICC yamuachiliwa huru rais wa zamani wa Kodivaa Laurent Gbagbo
https://parstoday.ir/sw/news/world-i50893-icc_yamuachiliwa_huru_rais_wa_zamani_wa_kodivaa_laurent_gbagbo
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ICC, imemuondoa hatiani na kumuachilia huru rais wa zamani wa Kodivaa Laurent Gbabgo ambaye alikuwa anakabiliwa na tuhuma za kuhusika katika ghasia za baada ya uchaguzi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jan 15, 2019 14:33 UTC
  • ICC yamuachiliwa huru rais wa zamani wa Kodivaa Laurent Gbagbo

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ICC, imemuondoa hatiani na kumuachilia huru rais wa zamani wa Kodivaa Laurent Gbabgo ambaye alikuwa anakabiliwa na tuhuma za kuhusika katika ghasia za baada ya uchaguzi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Majaji wa ICC wametoa hukumu ya kutaka Gbagbo, 73, aachiliwe huru pamoja na mpambe wake Charles Ble Goude. Wawili hao walikumbatiana baada ya hukumu hiyo huku wafuasi wao wakishangilia hapo mahakamani. Jaji Cuno Tarfusser amesema waliowengi katika jopo la majaji wamefikia natija kuwa kesi hiyo haikuwa na mashiko wala ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani wawili hao na hivyo kuamuru waachiliwe huru.

Wawili hao walkuwa wanakabiliwa na mashtaka ya jinai dhidi ya binadamu katika mwaka 2010-2011 katika vita vya ndani Kodivaa ambapo watu 3,000 waliuawa. Majaji wanasema hakuna ushahidi unaoonyesha wawili hao walipanga njama maalumu ya pamoja kutekeleza mauaji. Hata hivyo hawataachiliwa hadi kesho Jumatano ili kuupa upande wa mashtaka fursa ya kujibu hukumu hiyo.