China: Marekani itabeba dhima ya chochote kitakachotokea Venezuela
(last modified Tue, 29 Jan 2019 15:00:29 GMT )
Jan 29, 2019 15:00 UTC
  • China: Marekani itabeba dhima ya chochote kitakachotokea Venezuela

China sanjari na kutangaza uungaji mkono wake kwa Rais Nicolas Maduro wa Venezuela, imesema Marekani inapaswa kubebeshwa dhima kwa jambo lolote baya litakalotokea katika nchi hiyo ya Amerika ya Latini.

Geng Shuang, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema hatua ya Marekani kuiwekea vikwazo Venezuela haitakuwa na matokeo mengine ghairi ya kuyafanya maisha ya Wavenezuela kuwa mabaya zaidi.

Amesema China ilituma mjumbe maalumu wa Rais Xi Jinping kwenda nchini Venezuela kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Maduro.

Serikali ya Caracas imesema hatua hiyo ya Marekani ya kuiwekea Venezuela vikwazo vya mafuta ni njama ya kuiba mapato ya bidhaa hiyo muhimu inayoazalishwa kwa wingi nchini humo.

Rais Maduro na wanajeshi wa Venezuela

Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zimeipa Venezuela siku 8 kuitisha eti uchaguzi mwingine huru, vinginevyo zitamtambua kama rais Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani nchini Venezuela.

Hivi karibuni, China na Russia zilitumia kura ya veto kuzuia muswada uliowasilishwa na Marekani dhidi ya Venezuela katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Muswada huo wa Marekani ulikuwa na lengo la kumuunga mkono Juan Guaidó, spika aliyefutwa kazi na ambaye hivi karibuni alijitangaza kuwa rais wa mpito wa Venezuela. 

Tags