China na Russia zakosoa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel
(last modified 2024-10-10T07:13:03+00:00 )
Oct 10, 2024 07:13 UTC
  • China na Russia zakosoa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel

Wawakilishi wa Kudumu wa China na Russia katika Umoja wa Mataifa wameikosoa vikali Israel kwa kushindwa kutafuta amani na kuzuia juhudi za kukomesha mauaji ya watu wa Palestina.

Fu Cong, Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, jana Jumatano, aliutaka utawala wa Israel uondoe mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza na vizuizi vya upatikanaji wa misaada ya kibinadamu na kushirikiana kikamilifu na Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya masuala ya kibinadamu katika uwanja huo.

Fung Cong amesema suala la mauaji na njaa kufanywa kuwa jambo la kawaida katika Ukanda wa Gaza ni jambo lisilokubalika kabisa, na kusisitiza kuwa jamii ya kimataifa haiwezi kuruhusu mzozo huo uendelee na kupanuka na hatimaye kuitumbukiza Asia Magharibi nzima katika machafuko na vita.

Fu Cong

Kwa upande wake, Vasily Nebenzia, Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema Israel inadhoofisha kadhia ya Palestina kwa kupuuza maazimio ya Umoja wa Mataifa katika uwanja huo.

Nebenzia alisema katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba Israel inahujumu maamuzi ya mashirika ya kimataifa kwa kukataa kutekeleza azimio nambari 194 kuhusu wakimbizi, ambao ni msingi wa shughuli za Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).

Tangu 7 Oktoba mwaka jana, utawala ghasibu wa Israel ukiungwa mkono na Marekani, ulianzisha mauaji ya umati dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza ambapo umefanya uharibifu mkubwa katika ukanda huo na kutumia njaa kama chombo cha kuwaadhibu kwa pamoja maelfu ya Wapalestina. Wengi wao ambao ni wanawake na watoto, wameuawa shahidi na kujeruhiwa katika hujuma hiyo ya kinyama na inayokiuka sheria zote za kimataifa.

Tags