Russia: Huwenda hatutoyatambua matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/world-i52577-russia_huwenda_hatutoyatambua_matokeo_ya_uchaguzi_wa_rais_nchini_ukraine
Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Baraza la Shirikisho la Russia ameashiria uwepo wa ripoti zinazoonyesha kutokuwepo uzingatiaji wa sheria katika uchaguzi wa rais nchini Ukraine na kusema kuwa, huwenda serikali ya Moscow isitambue matokeo ya uchaguzi huo.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Apr 02, 2019 09:02 UTC
  • Russia: Huwenda hatutoyatambua matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Ukraine

Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Baraza la Shirikisho la Russia ameashiria uwepo wa ripoti zinazoonyesha kutokuwepo uzingatiaji wa sheria katika uchaguzi wa rais nchini Ukraine na kusema kuwa, huwenda serikali ya Moscow isitambue matokeo ya uchaguzi huo.

Konstantin Kosachev amesema kuwa, kutokana na maelfu ya ripoti za ukiukaji wa sheria baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais nchini humo, huwenda Russia ikakataa kuyatambua matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi. Ameongeza kwamba suala hilo linahusiana na uamuzi wa Rais Vladmir Puting wa Russia na chunguzi tofauti za kisiasa zitakazofanyika katika mabunge mawili ya nchi hiyo.

Rais Petro Poroshenko anayetetea nafasi yake na amabye ni adui wa Russia

Uchaguzi wa rais nchini Ukraine ulifanyika tarehe 31 Machi ambapo wagombea 39 walichuana kugombea nafasi hiyo. Volodymyr Zelensky mchekeshaji maarufu wa Ukraine na Petro Poroshenko wameingia duru ya pili ya uchaguzi huo baada ya kupata asilimia 30 na 17 ya kura. Kufuatia hali hiyo duru ya pili ya uchaguzi huo inatazamiwa kufanyika tarehe 21 Aprili mwaka huu.