Russia inataka kuwa mwanachama wa mfumo wa INSTEX
(last modified Sun, 30 Jun 2019 04:13:38 GMT )
Jun 30, 2019 04:13 UTC
  • Russia inataka kuwa mwanachama wa mfumo wa INSTEX

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa Moscow inataka kujiunga na mfumo maalumu wa mabadilishano ya kifedha kati ya Ulaya na Iran INSTEX kwa kifupi ili kufanya miamala yake ya kifedha na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Sergei Ryabakov amesema baada ya kumalizika kikao cha kamisheni ya pamoja ya makubaliano ya JCPOA huko Vienna Austria kuwa: Lililo na umuhimu ni kuandaa mazingira ya kutumiwa mfumo huu kwa nchi nyingine kwa kushirikiana na nchi zilizouanzisha na pia nchi saba za Ulaya ambazo zina uwezo wa kuandaa uwanja wa kutekelezwa suala hilo. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amekutaja kuanza kutumika mfumo wa INSTEX kuwa ni mwanzo wa njia na kusisitiza kuwa, mazingira mazuri yanapasa kuandaliwa kwa ajili ya kuwezesha ushirikiano wa kibiashara kati ya Iran na nchi nyingine. Kikao cha kamisheni ya pamoja ya JCPOA kilifanyika juzi Ijumaa huko Vienna nchini Austria. 

Bi Helga Schmid Naibu Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya alisema baada ya kufanyika kikao hicho kuwa Mfumo wa INSTEX umeanza kutekelezwa, na muamala wa kwanza umeshaanza kushughulikiwa.

Kamisheni ya pamoja ya makubaliano ya JCPOA kikaoni Vienna Austria