Wahajiri zaidi ya 500 wakwama katika pwani ya Ulaya
https://parstoday.ir/sw/news/world-i55355-wahajiri_zaidi_ya_500_wakwama_katika_pwani_ya_ulaya
Wahajiri haramu zaidi ya 500 ambao wako katika boti katika pwani ya Ulaya baada ya kuokolewa na huku boti hizo zikisubiri kuruhusiwa kutia nanga wamekwama katika bahari ya Mediterania.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 13, 2019 06:45 UTC
  • Wahajiri zaidi ya 500 wakwama katika pwani ya Ulaya

Wahajiri haramu zaidi ya 500 ambao wako katika boti katika pwani ya Ulaya baada ya kuokolewa na huku boti hizo zikisubiri kuruhusiwa kutia nanga wamekwama katika bahari ya Mediterania.

Televishni ya France 24 imeripoti kuwa, meli ya uokoaji ya Norway kwa jina la Ocean Viking hadi sasa imeokoa wahajiri haramu zaidi ya 350 hata hivyo nchi za Ulaya haziko tayari kuwapokea watu hao. 

Tatizo hilo limejitokeza siku chache baada ya Italia kutangaza kuwa itazitoza faini ya hadi pauni milioni moja ambayo ni sawa na dola zaidi ya milioni 1.1  meli ambazo zitabeba wahajiri na kujaribu kutia nanga katika bandari za nchi hiyo bila ya kibali. Serikali ya Italia aidha imeamuru kushikiliwa meli hizo na kumkamata mmoja wa manahodha wa meli hizo. 

Itakumbukwa kuwa, meli hizo ambazo zinasimamiwa na taasisi za kujitolea zinazotoa huduma za kibinadamu kwa kawaida hujishughulisha tu na masuala ya uokoaji katika maji ya kimataifa. Matteo Salvini Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu amekuwa akitumia lugha kali dhidi ya wahamiaji ili kujipatia umashuhuri na kuvutia uungaji mkono kwa chama chake cha League. Waziri huyo wa Mambo ya Ndani wa Italia aidha amekuwa mpangaji mkuu wa sera zenye lengo la kuzuia kupokelewa nchini humo wahajiri wowote kutoka eneo la Mashariki ya Kati na Afrika.

Matteo Salvini, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia 

Mwaka jana wa 2018 karibu wahajiri 3,800 ambao walikuwa na lengo la kuelekea nchi za Ulaya waliaga dunia katika bahari ya Mediterania.