Rais Nicolás Maduro: Hatuogopi hata kidogo kukabiliana kijeshi na Marekani
(last modified Tue, 18 Feb 2020 16:07:10 GMT )
Feb 18, 2020 16:07 UTC
  • Rais Nicolás Maduro: Hatuogopi hata kidogo kukabiliana kijeshi na Marekani

Rais Nicolás Maduro wa Venezuela sambamba na kufichua njama chafu za Rais Donald Trump wa Marekani kwa ajili ya kuishambulia kijeshi nchi hiyo ya Amerika ya Latini, amesisitiza kuwa nchi yake haitishiki na makabiliano ya kijeshi.

Rais Maduro ameyasema hayo alipokutana na jeshi la nchi hiyo na kuongeza kwa kusema: "Hatutaki vita, lakini pia hatuogopi makabiliano ya kijeshi, kama ambavyo tunadhamini usalama." Rais huyo wa Venezuela ameendelea kubainisha kwamba hivi sasa Trump amejiaminisha kuwa eti anaweza kuingia kirahisi kijeshi nchini Venezuela kwa kuwa anaandaa wapiganaji wake vibaraka kwa ajili ya kutekeleza shambulizi dhidi ya taifa hilo.

Rais Nicolás Maduro akiwa pamoja na askari wa Venezuela

Kadhalika Rais Nicolás Maduro amesema kuwa, kundi la askari waliokimbia jeshini wameweka kambi nchini Colombia na wanaendelea kupata mafunzo ili baadaye waweze kutekeleza shambulizi la kijeshi dhidi ya Venezuela. Inafaa kuashiriia kuwa serikali ya Marekani kwa kushirikiana na baadhi ya washirika wake, zinafanya juhudi kubwa zenye lengo la kuiondoa madarakani serikali halali ya Caracas. Mbali na vikwazo vingi na njama nyingi za kutaka kufanya mapinduzi ya kijeshi nchini humo, kadhalika Washington imetishia hata kutumia chaguo la kijeshi dhidi ya serikali ya nchi hiyo ya Amerika ya Latini.

Tags