Mar 04, 2020 13:16 UTC
  • Wahindu wenye kufurutu ada wachoma moto misikiti nchini India

Serikali ya India imefichua habari ya kuchomwa moto kikamilifu misikiti tisa na mamia ya nakala za Qur'an Tukufu katika shambulizi lililofanywa na Wahindu wenye misimamo mikali ya chuki dhidi ya Waislamu.

Gazeti la Times of India limeripoti Jumatano ya leo kwamba, misikiti iliyochomwa moto na Wahindu wenye kufurutu ada, ilikuwa misikiti mikubwa na muhimu New Delhi, mji mkuu wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa duru za kieneo, katika mashambulizi makali ya Wahindu wenye misimamo ya kigaidi kuwalenga Waislamu na yaliyodumu kwa siku kadhaa, kwa akali Waislamu 50 wameuawa na wengine zaidi ya 400 kujeruhiwa.

Sehemu ya ukandamizaji dhidi ya Waislamu nchini India

Video zilizosambaa kuhusiana na matukio hayo, zinaonyesha Wahindu makatili wakiwakandamiza Waislamu bila huruma, wakiwemo wanawake kwa kuwazika wakiwa hai, unyama ambao umeibua hasira kali ya Waislamu nchini India. Katika uwanja huo, hivi karibuni Abbas Mousavi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alielezea masikitiko yake kuhusiana na ukandamizaji wanaofanyiwa Waislamu nchini humo na kusema kuwa, Tehran inaitambua India kuwa nchi ya kuvumiliana kidini; hivyo habari za kuwepo ukandamizaji dhidi ya Waislamu nchini humo ni suala linalotia wasiwasi mkubwa.

Tags