China yakosoa uamuzi wa kivamizi wa utawala haramu wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/world-i60695-china_yakosoa_uamuzi_wa_kivamizi_wa_utawala_haramu_wa_kizayuni
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amekosoa vikali njama chafu za utawala haramu wa Kizayuni za kutaka kuyaunganisha maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 30, 2020 06:45 UTC
  • China yakosoa uamuzi wa kivamizi wa utawala haramu wa Kizayuni

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amekosoa vikali njama chafu za utawala haramu wa Kizayuni za kutaka kuyaunganisha maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Geng Shuang ameashiria suala hilo katika mazungumzo aliyofanya leo na waandishi wa habari mjini Beijing na kusema kuwa uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa kuyaunganisha maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi nyingine za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo ni jambo la kutia wasi wasi mkubwa na linalokwenda kinyume na sheria za kimataifa. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ameongeza kuwa, uamuzi wa Israel ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na azimio nambari 2234 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Netanyahu, Hitler wa zama hizi 

Kabla ya hapo pia Hami Aksoy, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki sambamba na kuashiria makubaliano ya hivi karibuni kati ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala Haramu wa Kizayuni na Benny Gantz, Mkuu wa Muungano wa Blu na Nyeupe, yanayolenga kuunganisha maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na maeneo mengine yanayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni, alisema kuwa hatua hiyo ni dhihirisho la fikra hatari ambayo inalenga kudhibiti ardhi zaidi za Wapalestina.