Venezuela yawakamata mamluki wa Marekani waliotaka kufanya mapinduzi
(last modified Tue, 05 May 2020 07:57:06 GMT )
May 05, 2020 07:57 UTC
  • Venezuela yawakamata mamluki wa Marekani waliotaka kufanya mapinduzi

Rais Nicolás Maduro wa Venezuela amesema vyombo vya usalama vya nchi hiyo vimewatia mbaroni 'magaidi' 13 wakiwemo mamluki wawili wa Kimarekani wanaohusishwa na jaribio lililotibuliwa la kujipenyeza nchini humo na kufanya mapinduzi.

Rais Maduro alisema hayo jana katika hotuba yake kwa taifa kwa njia ya televisheni, ambapo amewataja mamluki hao raia wa Marekani kama Airan Berry na Luke Denman wa kampuni ya Silvercorp yenye makao yake jimboni Florida nchini Marekani. 

Jordan Goudreau, Mkuu wa kampuni hiyo ya mamluki ya Florida Marekani ambayo huko nyuma ilikuwa ikifahamika kama Green Beret amekiri kuwa, raia hao wawili wa US ni sehemu ya wanaoendesha kile alichokitaja kama operesheni ya kuikomboa Venezuela.

Mamlaka husika nchini Venezuela imesema operesheni hiyo ya mapinduzi iliyopewa jina la "Operesheni Gideon" karibu na mji bandari wa La Guaira ilizimwa huku watu wanane wakiuawa.

Maandamano ya kutaka Marekani ikomeshe njama zake dhidi ya Venezuela

Wizara ya Ulinzi ya Venezuela imetoa taarifa ikivitaka vikosi vyote vya jeshi la nchi hiyo kujiweka tayari kwa ajili ya kuingia vitani kukabiliana na tishio la aina yoyote.

Katika miezi ya hivi karibuni, Marekani na washirika wake wamekuwa wakitekeleza njama za kufanya mapinduzi ya kijeshi kupitia kuwaunga mkono wapinzani wa serikali ya Caracas.

 

 

Tags